Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP)

MAADHIMISHO YA WIKI YA MSAADA WA KISHERIA MKOANI MBEYA

Leo tarehe 8/11/2021, TANLAP kwa kushirikiana na Mashirika wanachama, Serikali, wadau wa maendeleo na wananchi wa mkoa wa Mbeya wameshiriki uzinduzi wa Wiki ya Msaada wa Kisheria inayoadhimishwa kitaifa Mkoani Mbeya katika viwanja vya Ruanda- Nzovwe. Wiki ya Msaada wa Kisheria itaadhimishwa kuanzia tarehe 8/11 hadi 12/11/ 2021. Wiki ya Msaada wa Kisheria imezinduliwa na Mh. Juma Zuberi Homera- Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Katika uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANLAP, Ndugu Machumbana alipata fursa ya kueleza kwa Mgeni Rasmi kazi zinazofanywa na mtandao za uratibu wa shughuli za utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria nchini pamoja na Mradi wa MWANAMKE IMARA unaotekelezwa Mkoani Mbeya, Njombe na Kilimanjaro ukihusisha mashirika ya KWIECO, TANLAP, WiLDAF na TAWLA. Mashirika haya kupitia Mradi wa Mwanamke Imara yataendelea kutoa huduma ya msaada wa kisheria katika kipindi hiki cha maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria nchini.

Reach Us Today

4th Floor, Sky City Mall, Plot no. 403/1&3, Block A, Mlalakuwa
P.O. Box 33856
Dar es Salaam, Tanzania.
Tel:+255 22 2761806 /0746237265