Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP)

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA YA KUANZA USAJILI WA MASHIRIKA YANAYOTOA MSAADA WA KISHERIA CHINI YA SHERIA YA MSAADA WA KISHERIA, NA. 1 YA MWAKA 2017
Wizara ya Katiba na Sheria inapenda kuwataarifu kuwa, Usajili wa Mashirika yanayojihusisha na huduma ya Msaada wa Kisheria unaanza tarehe 25 mwezi
Julai 2018. Mwombaji anaweza kuwasilisha Maombi yake kwenye Ofisi za Wizara zilizopo Makao Makuu Dodoma kwenye anwani ifuatayo:
Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria cha Chuo Kikuu cha Dodoma
Jengo la Taaluma Na. 1
Barabara ya Mkalama
S.L.P 315
DODOMA
Maombi yatapokelewa pia kwenye Ofisi ndogo ya Wizara iliyopo Dar es salaam mkabala na jengo la Posta ya zamani, barabara ya Mkwepu, ghorofa ya 7.
Maombi yawasilishwe kwa mujibu wa Masharti ya Sheria na Kanuni, ikiwa ni pamoja na viambatisho yote muhimu kama ifuatavyo:
i. Fomu ya Maombi kama ilivyo kwenye Jedwali la Pili la Kanuni za Msaada wa Kisheria
ii. Taarifa ya kazi za Mwombaji
iii. Barua ya Utambulisho kutoka Ofisi ya Mkoa/Wilaya anamofanyia huduma
iv. Barua ya utambulisho kutoka Wizara /Ofisi iliyosajili Shirika (kama NGO, Kampuni, FBO, CBO nk)
Baada ya Maombi kukaguliwa na kuonekana yanakidhi vigezo vya usajili, Mwombaji atapaswa kufanya malipo ya usajili kwenye akaunti atakayopewa na
Wizara na kisha kupatiwa cheti cha usajili. Viwango vya ada ya usajili ni kama vilivyo kwenye Kanuni.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Ofisi ya Msajili kwa anwani ifuatayo:
registrar@sheria.go.tz
Imetolewa na Ofisi ya Msajili wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria

Reach Us Today

Biafra/Kanisani, Bwawani Street
Plot No. 434/42, Along Kawawa Road Kinondoni
P.O. Box 33856
Dar es Salaam, Tanzania.
Tel:+255 22 2761806