Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP)

WANAWAKE WANAONYANYASWA WATAKIWA KUTOA TAARIFA POLISI

WANAWAKE WANAONYANYASWA WATAKIWA KUTOA TAARIFA POLISI - Kamanda wa Polisi Dar, Lazaro Mambosasa amewataka Wanawake na Watoto wanaofanyiwa vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kuwasilisha malalamiko yao polisi - Mambosasa ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua semina ya Askari 160 kuwajengea uwezo kuhusu vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kwa Wanawake na Watoto - Amesema Wananchi hawatakiwi kubaki na maumivu moyoni wanapofanyiwa ukatili bali watoe taarifa Polisi kupitia dawati la kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto - Amesema Wanawake na watoto ni makundi yanayoathirika zaidi kwa unyanyasaji na kwamba Askari ni jukumu lao kusimamia sheria kuhakikisha makundi hayo yanalindwa Pia, aligusia baadhi ya makabila yenye mifumo dume kwa kunyanyasa Wanawake na Watoto, akibainisha kuwa mtazamo huo umekuwa ukileta shida katika kukemea vitendo hivyo. #16Days #HerSafetyMyResponsibility #UsalamaWakeWajibuWangu #TANLAP @unwomen @FCSTZ @USAID @FordFoundation @undo @OxfamTz @freedomhouse @OpenSocietyEA @IrlEmbTanzania @SwedeninTZ @undptz @IrlEmbTanzania @SayNO_UNiTE @canadaembassy @LSFTanzania @WiLDAFTz

Reach Us Today

Biafra/Kanisani, Bwawani Street
Plot No. 434/42, Along Kawawa Road Kinondoni
P.O. Box 33856
Dar es Salaam, Tanzania.
Tel:+255 22 2761806