+255 746 237 265

info@tanlap.or.tz

WANANCHI WAMEAMUA: PONGEZI KWA WALIOPIGA KURA

TANLAP inaishukuru Serikali kwa kutoa kibali cha uangalizi na kwa ushirikiano wakati wote wa kutimiza majukumu ya uangalizi. Pia inatoa pongezi kwa wananchi wote waliojitokeza kupiga kura na kwa wasimamizi wa uchaguzi waliofanya kazi yao kwa weledi.

TANLAP ilituma timu ya waangalizi wa uchaguzi yenye waangalizi 414 katika mikoa 26 na wilaya 184 Tanzania bara, ambao waliona kuwa kulikuwa na mwitikio kwa wananchi kujitokeza kupiga kura , hususan kutoka kwa makundi ya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu. Hii ni kutokana na juhudi za TANLAP kuendesha zoezi la utoaji elimu ya mpiga kura kwa kutumia wasaidizi wa kisheria waliopatikana nchi nzima, baada ya kuwapatia mafunzo ya kina. Aidha, TANLAP ilipata ushirikiano mzuri kutoka kwa Ofisi ya Rais - TAMISEMI katika kuhakikisha elimu hiyo inafika kwa wananchi wote.

Waangalizi waliripoti pia kuwa wananchi walihamasika kushiriki uchaguzi na kutumia haki yao ya kikatiba kwa ajili ya maendeleo ya maeneo yao. Hata hivyo, katika baadhi ya maeneo, walibaini changamoto, ambazo tunategemea Serikali itazifanyia kazi ili kuhakikisha kuwa katika chaguzi zijazo, mapungufu hayo hayajitokezi.

#WananchiTuamue