Orodha ya Mashirika Yaliyopata Kibali Cha Kutoa Elimu ya Mpiga Kura na Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu 2025
Description
Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 10(1) (g) (h) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya mwaka 2024 kikisomwa pamoja na Kanuni ya 22 ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za mwaka 2024, katika kikao chake maalum kilichofanyika tarehe 18 Julai, 2025 Tume imeridhia na kutoa kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2024 kwa taasisi na asasi za kiraia
164.
Aidha, kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 10(1)(i) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya mwaka 2024 kikisomwa pamoja na kifungu cha 85(4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024 na kanuni ya 13(1) na (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025 Tume, katika kikao hicho imeridhia na kutoa kibali cha uangalizi wa uchaguzi kwa taasisi na asasi 76 za ndani ya nchi na 12 za kimataifa.
Review
Login to Write Your ReviewThere are no reviews yet.