Go Back
Report Abuse

Sheria za Mirathi Zafanyiwa Mabadiliko Makubwa

0 (0 Reviews)
Screenshot 2025-07-22 100016
Screenshot 2025-07-22 100016

Description

Mheshimiwa Jaji Mkuu, George Masaju, (Jaji Mkuu mpya) ametumia mamlaka aliyopewa chini ya kifungu Cha 9 Cha Sheria ya Mirathi, (THE PROBATE AND ADMINISTRATION OF ESTATES ACT, CAP 352 R.E 2023) na mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya mahakama ya mahakimu, (section 71 of THE MAGISTRATE COURS ACT CAP 11 R.E 2023).

Ambapo kwa mujibu wa sheria hizo, Jaji Mkuu amepewa mamlaka ya kutunga kanuni zinazohusiana na masuala ya Mirathi. Na kwa mamlaka hayo ametunga kanuni mbili;

1. THE PROBATE (AMENDMENTS) RULES GN NO. 429 OF 2025

2. THE PRIMARY COURTS (ADMINISTRATION OF ESTATES) (AMENDMENTS) RULES GN NO. 428 OF 2025.

KWA HARAKA HARAKA MADALIKO YALIYOFANYIKA NI PAMOJA NA HAYA YAFUATAYO,

1. Kuanzisha akaunti rasmi ya Mirathi, 'special mirathi account'. Hivyo msimamizi wa mirathi anatakiwa kufungua akaunti ya benk yoyote maalumu kwaajili ya kukusanyia fedha za marehemu.

Miongoni mwa vipengere pia vilivyokuwa vinaleta shida ni pamoja na akaunti za kuweka fedha, Sasa wengi tulikuwa tunaambiwa tuweke kwenye akaunti ya mahakama. Uwekaji wa hela ulikuwa rahisi Ila utoaji wake ulikuwa na ukiritimba mwingi, Mara ziko hazina, Mara subiri siku kadhaa.

Hivyo ilitengeneza mianya ya rushwa, au hata kuwepo kwa akaunti zisizo rasmi wengine wakipewa akaunt binafsi

✓ Ewe msimamizi wa mirathi unatakiwa kufungua akaunti ya bank maalumu kwaajili ya Mirathi ya marehemu, na sio kutoa akaunti yako binafsi, au kutoa namba yako ya simu Kama akaunti hapana.

•Rejea Kanuni ya 2 ya GN no 428 of 2025 pamoja na kanuni ya 2(b) ya GN no. 429 of 2025.

2 Kubadili namba za Fomu zilizokuwa kwa kirumi na kuwa katika namba za kawaida.

Mara ya kwanza fomu za mahakama ya mwanzo za mirathi zilikuwa kwa kirumi, Fomu I, II, III, IV, V, VI ......

Lakini kwa Sasa tutatumia namba za kawaida, yaani FOMU 1,2,3,4, 5, 6 ......

Wale wa fomu maarufu fomu V na VI Sasa tutahamia na kutembea na fomu 5 & 6 si wote tunajua namba ya kirumi hizo.

3. Kubadilishwa kwa ada za mahakama kwenye masuala ya Mirathi.

Kanuni hii imeenda kufuta jedwali la pili, katika GN no. 429 of 2025.
Ambapo ada hizo ni kuanzia elfu 5 mpaka elefu 10 ndio kiasi Cha ada kilichopo kwa Sasa.

4. Mabadiliko kwenye jedwali la kwanza (Kubadilishwa na kufuatwa kwa baadhi ya fomu)

Mfano, FOMU 2, 6, 18, 26,25, 63, 66, 67 .. na zingine Kuna madadiliko makubwa kwenye fomu hizo,
fomu 18, 26 za kuomba kuwa msimamizi wa mirathi Kuna madadiliko hapa angalia vyema kabla ya kupeleka maombi mahakamani.

Fomu 67, inahusu kuhamisha fedha kwenda kwenye akaunti maalumu ya Mirathi

•Rejea GN no 429 ya mwaka 2025.

5.Kupunguzwa ukomo wa muda, Kutoka miaka 3 Sasa ni miezi 12

Ukisoma kanuni ya 31(1) ya Mirathi, ilikuwa ikieleza ukomo wa muda kwenye kufungua mirathi, ambapo ilikuwa miaka mitatu, lakini kwasasa imepunguzwa na kuwa miezi 12 yaani mwaka mmoja

Hivyo marehemu akifariki ikapita miezi 12 hujaomba mirathi ukiomba baada ya muda huo kuisha, ieleze mahakama sababu za kuchelewa kufungua shauri. Wataalamu wa P.O chukua silaha yenu hii😊

Rejea Kanuni ya 17 ya GN No. 429 of 2025, Soma pamoja Kanuni ya 3 ya GN No.428 of 2025

6. Muda wa kufile fomu ya hesabu za mirathi 'Fomu 6' / hesabu za mgawanyo wa mirathi Sasa ni miezi mitatu (3) badala ya miezi minne (4) ya mwanzo.

Rejea kanuni ya 8 ya GN 428 OF 2025

7. Baadhi ya maombi Sasa kufanyika kwa njia moja wapo kati ya barua, maombi ya mdomo, nyaraka maalumu, (maombi ya faradha pamoja na kiapo chake/fomu maalumu, wataalamu wanasema chamber summons + affidavit).

 

There are no reviews yet.

About TANLAP

we build the capacity of legal aid providers, harmonize service quality and ethics, and advocate for rights-based law and policy reforms.

Through partnership, innovation, and unwavering integrity, TANLAP strengthens grassroots voices and drives systemic change so that every Tanzanian can seek and obtain fair legal remedies.

Reach Us

© 2025| All rights reserved - Tanzania Network of Legal Aid Providers