Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP)

News

Post date: Thu, 03/05/2020 - 19:48
Comments: 0

Huduma za msaada wa kisheria zikiendelea hapa Ngara na wananchi wameendelea kujitokeza kwa wingi kupata huduma ya msaada wa kisheria kwenye maswala mbalimbali yakiwemo ardhi, mirathi, ndoa na mashauri mengine mengi.

Post date: Thu, 03/05/2020 - 19:29
Comments: 0

Mkuu wa Wilaya ya Ngara akitoa hotuba na salamu za shukrani kwa TANLAP na UN Women katika uwanja wa Posta ya zamani Wilayani Ngara Mkoani Kagera. Ziara ya TANLAP mkoani Kagera inaendelea na utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi wa Ngara.

Post date: Tue, 03/03/2020 - 19:22
Comments: 0

Wananchi kutoka sehemu mbalimbali wilayani Karagwe wakipatiwa huduma ya Msaada wa Kisheria katika viwanja vya Kayanga.

Post date: Tue, 03/03/2020 - 19:20
Comments: 0

TANLAP kupitia ufadhili wa UN WOMEN leo imezindua wiki ya Msaada wa Kisheria wilayani Karagwe mkoa wa Kagera kuelekea siku ya mwanamke duniani. Uzinduzi huo umefanywa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brig. Gen. Marco Gaguti na kuhudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Karagwe, Katika salamu zake, Mkuu wa Mkoa amewasisitiza wananchi wa Karagwe waje kwa wingi kupata elimu ya sheria na kupata huduma ya msaada wa kisheria inayotolewa bure katika viwanja vya Kayanga. Pia amewaasa wananchi kuibua na kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia kwenye vyombo husika na kuepuka kujichukulia sheria mkononi.

Pages

Reach Us Today

Biafra/Kanisani, Bwawani Street
Plot No. 434/42, Along Kawawa Road Kinondoni
P.O. Box 33856
Dar es Salaam, Tanzania.
Tel:+255 22 2761806 /0746237265