Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP)

Huduma ya Msaada wa Kisheria mkoani Njombe

Katika kuendeleza maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria iliyozinduliwa Mkoani Mbeya tarehe 8/11 kwenye viwanja vya Ruanda- Nzovwe, TANLAP kwa kushirikiana na wanachama wake TAWLA, WiLDAF, KWIECO pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa wameweza kutoa elimu ya kisheria na huduma ya msaada wa Kisheria Mkoani Njombe, Wilaya ya Ludewa, Kata ya Mavanga, Kijiji cha Mavanga. Tukio hili limefanyika tarehe 10/11/2021 katika viwanja vya Kata - Mavanga kama sehemu ya shughuli za Mradi wa Mwanamke Imara unaolenga kuwakinga Wanawake na vijana dhidi ya ukatili wa kijinsia kupitia huduma ya Msaada wa Kisheria.

Reach Us Today

4th Floor, Sky City Mall, Plot no. 403/1&3, Block A, Mlalakuwa
P.O. Box 33856
Dar es Salaam, Tanzania.
Tel:+255 22 2761806 /0746237265