


Tarehe 29 Septemba, 2025 TANLAP ilitoa elimu ya mpiga kura kwa watu wenye ulemavu katika kata ya Segerea jijini Dar es salaam. Washiriki kutoka katika mitaa yote ya kata hiyo walijitokeza kwa wingi kusikiliza elimu ya mpiga kura,miongoni mwa masuala muhimu yaliyogusiwa ni namna watu wenye ulemavu wanavyopewa kipaumbele katika mchakato wa uchaguzi.
Mwezeshaji kutoka TANLAP Wakili Fransisca Silayo alifundisha mada mbalimbali ikiwepo umuhimu wa kushiriki katika kampeni ili kusikiliza sera za wagombea na kuwasisitiza kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura siku ya uchaguzi tarehe 29 Octoba.
Elimu hiyo imetolewa katika ukumbi wa ofisi za kata ya Segerea.